• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa Uingereza apongeza uhusiano mzuri baina ya nchi yake na China

    (GMT+08:00) 2016-09-05 09:35:38
    Waziri mkuu wa Uingereza Bibi Theresa May amesema, uhusiano baina ya nchi yake na China upo katika kipindi muhimu kizuri, na kwamba atatumia fursa ya mkutano wa kilele wa G20 kuwaoneshea viongozi wa nchi mbalimbali ishara chanya kwamba Uingereza itaendelea kuwa na uwazi ulio nao siku zote.

    Bi May anatarajiwa kukutana na rais Xi Jinping wa China wakati wa mkutano huo, ambapo itakuwa ni mara ya kwanza kwa wakuu hao wawili kukutana tangu serikali mpya ya Uingereza iundwe.

    Bi May pia atazungumza na viongozi wa nchi mbalimbali kuhusu makubaliano mapya ya biashara baada ya Uingereza kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya, na kusisitiza dhamira ya Uingereza ya kuongoza biashara huria duniani.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako