• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa kilele wa Kundi la G20 wafungwa Hangzhou, China

  (GMT+08:00) 2016-09-05 21:56:07
  Awamu ya 11 ya mkutano wa kilele wa Kundi la nchi 20 umefungwa leo alasiri mjini Hangzhou, China.  Rais Xi Jinping wa China ambayo ni nchi mwenyeji wa mkutano huo, amekutana na waandishi wa habari akieleza matokeo yaliyopatikana kwenye mkutano huo.

  Rais Xi Jinping amesema, washiriki wote wa mkutano huo wameonesha dhamira ya kupanga njia ya maendeleo ya uchumi wa dunia, kufanyia uvumbuzi mbinu za kutimiza maendeleo, kukamilisha usimamizi wa kiuchumi na kifedha duniani, kufufua tena biashara na uwekezaji wa kimataifa ambazo ni injini mbili muhimu za ukuaji wa uchumi wa dunia, na vilevile kusukuma mbele maendeleo yenye ushirikishi na muungano, ili kuyawezesha matokeo ya ushirikiano wa kundi la G20 yanufaishe dunia nzima.

  Kwenye mkutano na waandishi wa habari baada ya kufungwa kwa mkutano wa G20 mjini Hangzhou, rais Xi amesema, mkutano huo umetimiza malengo yaliyowekwa.

  "Mkutano wa kilele wa G20 wa Hangzhou umefanyika katika kipindi muhimu kwa ukuaji wa uchumi wa dunia na mageuzi ya kundi la G20. Ufufukaji wa uchumi wa dunia umekuwa dhifu, masuala makubwa ya kimataifa na ya kikanda pamoja na changamoto zinazoikabili dunia vimetoa athari dhahiri kwa uchumi wa dunia, na hatari na hali mbalimbali zisizotabirika bado zinajitokeza, kwa hivyo mkutano huo umefuatiliwa sana kwenye jumuiya ya kimataifa, na pia umebeba matarajio makubwa ya pande mbalimbali. Kutokana na juhudi za pamoja za nchi wanachama wa G20, nchi wageni na mashirika ya kimataifa, mkutano huo umepata matokeo mengi na umetimiza malengo yaliyowekwa."

  Chini ya kaulimbiu ya "Kujenga uchumi wa dunia unaoungana wenye uvumbuzi, uhai na ushirikishi", washiriki wa mkutano huo wamebadilishana kwa kina maoni, ambapo wamethibitisha mwelekeo, malengo na hatua za ushirikiano wa G20 na kufikia makubaliano kuhusu kuhimiza ukuaji wa uchumi wa dunia. Rais Xi amesema, pande zote zimekubali kuwa kulinda mazingira ya kimataifa yenye amani na utulivu kuna umuhimu mkubwa katika kukabiliana na hatari na changamoto zinazoikabili dunia ya leo.  

  "Kundi la G20 linapaswa kuenzi moyo wa wenzi wa kusaidiana, kuimarisha zaidi uratibu wa kisera, kutekeleza mpango wa utekelezaji wa Hangzhou, na kutumia kwa njia mwafaka mbinu za kisera zikiwemo sera za kifedha, za kisarafu na mageuzi ya kimuundo, si kama tu linatakiwa kuwa tayari kuzuia na kukabiliana na hatari za muda mrefu, bali pia linapaswa kutilia maanani kujenga mustakbali wa ukuaji kwa kipindi kirefu, si kama tu linatakiwa kupanua mahitaji ya jumla, bali pia linapaswa kuzidisha ubora wa ugavi. Tuna imani kwamba kwa kupitia juhudi za pamoja za pande mbalimbali, tutaweza kuurejesha uchumi wa dunia kwenye njia sahihi ya ukuaji endelevu wenye uwiano na ushirikishi."

  Imefahamika kuwa, mwaka kesho Ujerumani itapokea zamu kutoka China kuwa nchi mwenyekiti wa G20, na kuandaa mkutano wa kilele wa G20 huko Hamburg.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako