• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa G20 wapata mafanikio makubwa

    (GMT+08:00) 2016-09-06 10:17:41

    Mkutano wa wakuu wa kundi la nchi 20 (G20) ulimalizika jana huko Hangzhou China kwa makubaliano mengi yaliyofikiwa kati ya viongozi mbalimbali.

    Akiongelea mkutano huo, Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amesema,

    "Mkutano huo uliofanyika hapa Hangzhou umekuwa wa ufanisi na umefuatilia masuala yanayohusu dunia nzima. Mageuzi yamekuwa ajenda muhimu ya mkutano huu ili kudumisha ongezeko endelevu na shirikishi la uchumi wa dunia kwa muda mrefu na kwa usawa. Pande mbalimbali zimeafikiana juu ya masuala mengi yakiwemo uvumbuzi na usawazishaji wa sera za udhibiti na marekebisho ya uchumi. "

    Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF Bi. Christine Lagarde amesema mkutano huo umekidhi matarajio ya watu kuhusu kushughulikia kwa ufasaha hatari na changamoto zinazoukabili uchumi wa dunia.

    "MKutano wa wakuu wa kundi la nchi 20 ulifanyika wakati kasi ya ukuaji wa uchumi wa dunia ikiwa ni ndogo, na watu wachache kunufaika na ukuaji huo. Pande mbalimbali zimefikia makubaliano muhimu kwamba tunahitaji ukuaji wa uchumi, na ukuaji huu unatakiwa kuwa shirikishi. Tunaunga mkono kuhimiza ukuaji kwa kutumia sera za kifedha na mageuzi ya muundo. Na makubaliano kuhusu ukuaji shirikishi yamekidhi matarajio ya watu ambao wanaona hawajanufaika na ukuaji wa uchumi."

    Licha ya kutafuta njia za kuhimiza ukuaji wa uchumi wa dunia, mkutano huo pia umetoa taarifa ya mwenyekiti kuhusu suala la mabadiliko ya hali ya hewa ambayo ni taarifa ya kwanza kuhusu suala hilo katika historia ya mkutano wa wakuu wa G20. Rais Francois Hollande amesema,

    "Mkutano huo umesisitiza kuwa kuanzia mwaka 2020 nchi zilizoendelea zitatoa dola za kimarekani bilioni 100 katika kusaidia nchi zinazoendelea na mahitaji yao katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kutimiza maendeleo endelevu. Wakati huo huo, mkutano huo pia umehimiza serikali za nchi mbalimbali, mashirika ya kimataifa na sekta binafsi kutoa uungaji mkono wa kifedha kwa ajili ya matumizi zaidi ya nishati safi duniani. Hili ni suala muhimu sana hasa kwa nchi zinazoendelea."

    Mkutano wa G20 umemalizika, lakini kutokana na juhudi za pamoja za pande mbalimbali, mwisho wa mkutano huo unatarajiwa kuwa mwanzo mpya wa ushirikiano unaoelekea ukuaji wa uchumi wa dunia wenye nguvu na uwiano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako