• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa kilele wa G20 wa Hangzhou watoa "ufumbuzi wa kichina" kwa usimamizi wa kiuchumi duniani

    (GMT+08:00) 2016-09-06 21:06:09

    Mkutano wa 11 wa kilele wa kundi la nchi 20 ulifungwa jana huko Hangzhou, China. Wakati ufufukaji wa uchumi wa dunia ukiwa dhaifu na nchi mbalimbali zote zinatafuta mbinu za kuchochea ukuaji wa uchumi, China ikiwa ni nchi mwenyekiti wa mkutano huo, imetoa ufumbuzi wa kichina kwa ajili ya usimamizi wa kiuchumi duniani. Taarifa ya mkutano wa kilele wa G20 wa Hangzhou inaonesha kuwa ufumbuzi huo umekubaliwa na pande nyingi.

    Ajenda muhimu za mkutano huo ni pamoja na kuimarisha uratibu wa kisera, kufanyia uvumbuzi njia za kujiendeleza, na usimamizi wenye ufanisi wa mambo ya kiuchumi na kifedha duniani, uwekezaji na biashara ya kimataifa na maendeleo yenye ushirikishi na muungano. Matokeo yaliyopatikana kwenye mkutano huo yamefuatilia kwa karibu masuala hayo.

    Hivi sasa tofauti kubwa kati ya sera za kiuchumi zinazotekelezwa na makundi makuu ya uchumi duniani, imeleta hali isiyotabirika kwa uchumi wa dunia. Kwa hivyo mkutano huo umesisitiza zaidi uratibu wa kisera na kutilia maanani sera za mageuzi ya kimuundo. Mkurugenzi wa idara ya utafiti katika kituo cha mawasiliano ya kiuchumi cha kimataifa cha China Bw. Xu Hongcai amesema, mkutano huo utatoa mchango mkubwa katika kuimarisha uratibu wa kisera kati ya nchi wanachama wa G20, na vilevile utasisitiza zaidi umuhimu wa mageuzi ya kimuundo katika kuhimiza ukuaji wa uchumi kwa muda mrefu.

    "Umaalamu mkubwa wa mkutano wa mwaka huu ni kwamba uratibu wa kisera kati ya nchi zenye uchumi mkubwa umepewa kipaumbele, ambao unahusisha sera za kifedha, kisarafu na za mageuzi ya kimuundo. Mkutano huo pia umesisitiza mageuzi ya muundo wa kiuchumi, kwa mfano wa mageuzi ya kimuundo yanayoendelea nchini China. Katika miaka ya karibuni, nchi zilizoendelea kama vile Marekani na nchi za Ulaya pia zimeanza mageuzi ya kimuundo, kuna maoni ya pamoja kuhusu suala hili."

    Kwenye mkutano huo viongozi wa G20 wameidhinisha sekta 9 zinazopewa kipaumbele ambazo zilithibitishwa kwenye ajenda ya G20 ya kuimarisha mageuzi ya kimuundo, pamoja na kanuni mbalimbali za mwongozo.

    Hivi sasa uchumi wa dunia uliokwama unahitaji nguvu mpya ya msukumo. Kwenye mkutano huo wa G20, China kwa mara ya kwanza imeweka "kufanyia uvumbuzi njia ya kujiendeleza" kwenye ajenda kuu za mkutano huo. Taarifa ya mkutano huo inaonesha kuwa, Mpango wa G20 wa kufanya uvumbuzi kwa mbinu za kutimiza maendeleo ulioidhinishwa na viongozi wa kundi hilo umejumuisha sera na hatua zinazohusisha uvumbuzi, mapinduzi mapya ya kiviwanda na uchumi wa kidijitali. Mbali na hayo, G20 pia imethibitisha umuhimu wa mageuzi ya kimuundo. Mtafiti wa taasisi ya utafiti wa mahusiano ya kimataifa ya China Chen Fengying amesema, matokeo hayo yatatoa fursa mpya za maendeleo kwa uchumi wa dunia.

    "Kufanyia uvumbuzi njia za kujiendeleza kiuchumi kunahitaji uvumbuzi wa sayansi na teknolojia, uvumbuzi wa kimfumo na uvumbuzi kwa mawazo ya kisoko, kwa hivyo kunahusisha mapinduzi mapya ya kiviwanda, uchumi wa kidijitali, cloud computing na biashara ya kimataifa kwenye mtandao wa Internet na kadhalika. Inavyotakiwa ni kuwa na wazo jipya, nadharia mpya, mtizamo mpya na teknolojia mpya, ili uchumi wa dunia uweze kupata msukumo mpya na uhai mpya."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako