• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China ahudhuria mkutano kati ya China na ASEAN

    (GMT+08:00) 2016-09-07 19:21:02

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang leo asubuhi amehudhuria mkutano wa 19 wa viongozi wa China na Jumuiya ya nchi za Asia ya kusini mashariki ASEAN, na mkutano wa kilele wa kuadhimisha miaka 25 ya uhusiano wa mazungumzo kati ya China na ASEAN, uliofanyika huko Vientiane nchini Laos.

    Kwenye mkutano huo, waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amesema, katika miaka 25 iliyopita uhusiano kati ya China na ASEAN umepata mafanikio mengi na China inapenda kushirikiana na nchi za ASEAN katika kuimarisha mawasiliano ya kimkakati na kuhimiza ushirikiano.

    "Kama ni umri wa mtu miaka 25 ni kipindi cha ukuaji, na sasa tumeanza kuelekea kupevuka. Tangu China na ASEAN zianzishe uhusiano wa mazungumzo mwaka 1991, siku zote pande hizi mbili zimeshikilia mtizamo wa kuhimiza ushirikiano wa kunufaishana, na uhusiano kati ya pande hizo mbili umejengwa kwenye msingi wa kuheshimiana, kuelewana, kuaminiana na kuungana mikono. Hali hii imeufanya uhusiano huu upige hatua kubwa mbele, na kuhimiza kidhahiri amani na utulivu, na vilevile maendeleo na ustawi wa kanda hiyo."

    Bw. Li Ke qiang amesema, miaka 25 iliyopita ni kipindi ambacho China na ASEAN zimeendelea kuimarisha uaminifu wa kisiasa. China ni nchi ya kwanza kujiunga na Mkataba wa urafiki na ushirikiano kati ya nchi za Asia ya Kusini mashariki, ni nchi ya kwanza kueleza msimamo wa wazi wa kuunga mkono hadhi ya uongozi ya ASEAN kwenye ushirikiano wa kikanda, ni nchi ya kwanza kuanzisha uhusiano wa wenzi wa kimkakati na ASEAN, ni nchi ya kwanza kueleza wazi nia ya kusaini Mkataba wa maeneo yasiyo na silaha za nyuklia katika Asia ya kusini mashariki na ASEAN, na pia ni nchi ya kwanza kuanzisha mchakato wa mazungumzo ya biashara huru na ASEAN. Bw. Li Keqiang amesema,

    "Mambo haya yanaonesha kwamba China na ASEAN zimekuwa na uaminifu wa kisiasa, hasa pande hizo mbili zina ushirikiano mkubwa wa kunufaishana na mawasiliano ya karibu ya watu. Tunaweza kusema nafasi hizo za kwanza zilizochukuliwa na China zimeonesha nia ya China ya kupenda kufanya ushirikiano wa kunufaishana na nchi jirani haswa nchi za ASEAN. Sote tunatarajia mazingira yenye amani na utulivu, na sote tunapenda kuwa na majirani wema ambao uchumi wao unaweza kunufaishana na tamaduni zao zinaweza kuingiliana."

    Bw. Li Keqiang amesema, uhusiano kati ya China na ASEAN una mustakbali mkubwa, na China siku zote inaichukulia ASEAN kuwa ni nguvu muhimu ya kulinda amani na utulivu wa kanda hiyo na kuhimiza utandawazi wa kikanda na maendeleo ya dunia yenye ncha nyingi. Amesisitiza kuwa China intaendelea kutoa kipaumbele kwa ASEAN katika diplomasia zake na nchi jirani, kuunga mkono hadhi muhimu ya ASEAN kwenye ushirikiano wa kikanda na vilevile kuiunga mkono ASEAN ichukue nafasi kubwa zaidi kwenye mambo ya kikanda na ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako