• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa pili wa Baraza la uwekezaji kwa Afrika wafunguliwa Guangzhou

    (GMT+08:00) 2016-09-08 20:51:44

    Mkutano wa pili wa Baraza la uwekezaji kwa Afrika ulifunguliwa jana mjini Guangzhou, China. Kwenye mkutano huo, naibu waziri mkuu wa China Bw. Ma Kai amependekeza kupanua maeneo ya ushirikiano wa uwekezaji kati ya China na Afrika, na kusisitiza kuwa China inapenda kufanya ushirikiano halisi na nchi za Afrika kwenye sekta mbalimbali, ili kuunganisha sekta bora, raslimali bora na mifumo bora ya pande hizo mbili.

    Katika miaka zaidi ya kumi iliyopita, ushirikiano kati ya China na Afrika umepiga hatua kubwa na kwa kasi, na China imekuwa mwenzi wa kwanza wa kibiashara wa Afrika kwa miaka 7 mfululizo. Hivi sasa makampuni zaidi ya 3,000 ya China yamewekeza au kushiriki kwenye ujenzi wa miundombinu ya umeme, nishati, mawasiliano na huduma za jamii barani Afrika. Mwaka huu ukiwa ni mwaka wa 60 tangu China na Afrika zianzishe uhusiano wa kidiplomasia, naibu waziri mkuu wa China Bw. Ma Kai amesema, baada ya maendeleo ya miaka 60, hivi sasa uhusiano kati ya China na Afrika umefika kwenye mwanzo mpya wa kihistoria.

    "Afrika iko kwenye kipindi muhimu cha ukuaji wa uchumi, ambapo mchakato wa kukuza viwanda na kuendeleza miji barani Afrika umeharakishwa, ujenzi wa miundombinu ya kimsingi unaendelea kwa kufuata utaratibu, na mahitaji ya ushirkiano na nje yamezaidi kuongezeka. China ina mfumo kamili wa viwanda na uwezo wa kutengeneza vifaa mbalimbali, ina nguvu kubwa ya mitaji, teknolojia na soko, pamoja na uwezo wake mkubwa wa kujenga miundombinu ya kimsingi na uzoefu mwingi wa usimamizi wa maeneo ya viwanda. Pande hizo mbili zinaweza kutumia nguvu zao bora kwenye ushirikiano wa uwekezaji na biashara, ili kutimiza maendeleo yanayonufaisha pande zote mbili."

    Bw. Ma Kai anaona kuwa ushirikiano wa pande zote kati ya China na Afrika kwenye msingi wa usawa na kunufaishana si kama tu umeimarisha urafiki kati yao na kuleta manufaa kwa watu wao, bali pia umeihimiza jumuiya ya kimataifa ifuatilie na kuwekeza zaidi barani Afrika, hali inayoufanya kuwa mfano wa kuigwa wa Ushirikiano wa Kusini na Kusini. Bw. Ma Kai amependekeza kupanua zaidi maeneo ya uwekezaji kati ya China na Afrika.

    "China itashiriki kwenye ujenzi wa kilimo na viwanda vya kisasa barani Afrika. China itaimarisha ushirikiano na Afrika kwenye sekta mbalimbali, haswa sekta ya utengenezaji bidhaa inayohitaji nguvu kazi nyingi, China pia itahimiza mageuzi ya sekta za nishati na rasilimali, ili kuisaidia Afrika kuinua uwezo wake wa kutimiza maendeleo endelevu. Vilevile China itashiriki kwenye ujenzi wa miundombinu ya kimsingi ikiwemo barabara, reli, mawasiliano ya habari na umeme, na kuunga mkono mafunzo ya kuandaa wataalamu na kuhimiza ushirikiano wa uwekezaji kwenye sekta za afya, utamaduni na elimu. Pia tunakaribisha makampuni ya Afrika kushiriki kwenye mageuzi ya kimuundo na kiviwanda nchini China. China inapenda kufanya ushirikiano halisi wa muda mrefu na nchi za Afrika, ili kuunganisha sekta bora, raslimali bora na mifumo bora ya pande hizo mbili."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako