• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chombo cha Philae kilichopotea baada ya kutua kwenye kimondo katika miaka miwili iliyopita kimegunduliwa tena

    (GMT+08:00) 2016-09-09 10:11:07

    Idara ya anga ya juu ya Ulaya ESA imetangaza kuwa tarehe 2 chombo cha uchunguzi cha Rosetta kilipiga picha za chombo cha Philae kilichokwama ufani kwenye kimondo cha Churyumov-Gerasimenko kwa bahati.

    Mwaka 2004 chombo cha uchunguzi cha Rosetta kikibeba chombo cha Philae kilirushwa angani. Baada ya kusafiri kwa muongo mmoja, tarehe 12 Novemba mwaka 2014, chombo cha Philae kilitoka kwenye chombo cha Rosetta na kutua kwenye kimondo cha Churyumov-Gerasimenko, lakini hakikutua kwa mafanikio na kuanguka kando ya shimo moja. Kivuli cha shimo hili kilizuia betri za nishati ya jua kupata mwanga wa jua wa kutosha, na chombo hiki hakikufanya kazi baada ya siku tatu. Baadaye kimondo hiki kilielekea kenye jua siku hadi siku, na baada ya kupata mwanga mwingi zaidi wa jua, chombo hiki kilifanya kazi tena na kutuma data duniani kwa mara kadhaa kuanzia mwezi Juni hadi Julai mwaka 2015, lakini baadaye kilikuwa kimya tena.

    Philae ni chombo cha kwanza kilichotua kwenye kimondo cha Churyumov-Gerasimenko. Kutua kwenye kimondo hiki ni sehemu moja ya mradi wa uchunguzi wa kimondo wa Rosetta. Wanasayansi wanatarajia kutafiti chanzo cha mfumo wa jua na viumbe kupitia mradi huo.

    Kwa mujibu wa mpango wa ESA, mradi wa Rosetta utamalizika tarehe 30 mwezi huu. Wakati huo chombo cha Rosetta kitafanya kazi ya mwisho, yaani kugonga eneo lenye mashimo mengi, ili kufichua muundo wa ndani wa kimondo hiki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako