• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii ( Septemba 3-Septemba 9)

    (GMT+08:00) 2016-09-09 19:50:28

    EAC yakubali mapendekezo ya mratibu wa mazungumzo ya Burundi

    Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC wameiomba Jumuiya ya kimataifa kusaidia na kufadhili mchakato wa mazungumzo ya amani kuhusu Burundi, wakati huu wakiidhinisha mapendekezo ya mratibu wa mazungumzo hayo Rais wa zamani wa Tanzania, Benjamin Mkapa.

    Akizungumza jijini Dar es Salaam, wakati wa kuhitimisha mkutano maalumu wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, Rais wa Tanzania na mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, John Pombe Magufuli, amesema wanaunga mkono juhudi za mratibu wa mazungumzo hayo na mpatanishi wa mgogoro wa Burundi, Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni.

    Rais Magufulu amesema kuwa, walipokea taarifa ya mratibu wa mazungumzo ya amani ya Burundi, Rais Mkapa, ambaye tayari ameshazikutanisha pande zinazokinzana nchini Burundi katika mazungumzo aliyoyafanya jijini Arusha na Brussels.

    Viongozi hao wameitaka Jumuiya ya Kimataifa ukiwemo umoja wa Ulaya, kusaidia kifedha mchakato wa mazungumzo hayo, ambayo wamesema bila ya uwezeshwaji wa kutosha huenda wasifikie malengo, huku wakisisitiza imani yao kwa mratibu wa mazungumzo na hatua ambazo ameshazichukua hadi sasa.

    1 2 3 4 5 6 7 8
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako