• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii ( Septemba 3-Septemba 9)

    (GMT+08:00) 2016-09-09 19:50:28

    Maaskofu DRC wasisitiza umuhumi wa mazungumzo shirikishi

    Baraza la kitaifa la Maaskofu wa kanisa katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, limesisitiza wito wake juma hili wa kuwa na mazungumzo ya kitaifa ambayo yanashirikisha pande zote na kwa kuzingatia katiba ya nchi.

    Katika taarifa yao kwa vyombo vya habari iliyotolewa Jumanne ya September 6, baraza hilo la maaskofu, linasema kuwa kamwe haliwezi kushiriki kwenye mazungumzo ya kitaifa yanayoendelea hivi sasa ikiwa masuala haya muhimu waliyoyaeleza hayakuzingatiwa.

    Taarifa yao imeongeza kuwa, kwa kuwa na mazungumzo ya kweli na ya wazi ambayo yatasababisha kumalizika kwa mzozo wa kisiasa kwenye taifa hilo, baraza lao lina waalika wadau wote nchini humo ilikuwa kuwa na changanyiko shirikishi.

    Baraza la Maaskofu linasema kuwa, wao wanaamini kushirikishwa kwa viongozi wa kuu na muhimu wa upinzani kwenye mazungumzo hayo, kutatoa nafasi kwa nchi hiyo kufikia malengo ya kutatua kasoro ambazo zinashuhudiwa kwa sasa.

    Hata hivyo maaskofu hao wametaka kuachiwa kwa wafungwa zaidi wa kisiasa bila kuwataja majina.

    Maaskofu hao wameongeza kuwa, mazungumzo ni lazima yafanywe kwa kuzingatia na kuheshimu katiba ya nchi, na kusisitiza kuhusu kuheshimiwa kwa kipengele ambacho kinahusu muhula wa rais kukaa madarakani na kukabodhi madaraka kidemokrasia.

    1 2 3 4 5 6 7 8
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako