• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii ( Septemba 3-Septemba 9)

    (GMT+08:00) 2016-09-09 19:50:28

    AU yaahirisha kutuma ujumbe Gabon

    Umoja wa Afrika umeahirisha kutuma ujumbe wake utakaohusika na kuchangia kutatua mgogoro wa kisiasa nchini Gabon.

    Waziri wa mambo ya Nje wa Gabon, Emmanuel Isozet Ngondet, ametangaza Alhamisi kwamba Umoja wa Afrika haujaleza tarehe nyingine ya kutuma ujumbe huo.

    Wapatanishi wa Umoja wa Afrika walikua wakitarajiwa kuwasili mjini Libreville, mji mkuu wa Gabon, Ijumaa, Septemba 9, kujadili na wahusika wakuu wa mgogoro wa kisiasa nchini humo.

    Wakati huo huo rais mteule wa Gabon, Ali Bongo Ondimba, amewatuhumu waangalizi wa uchaguzi kutoka umoja wa Ulaya, ambao wameukosoa uchaguzi uliofanyika nchini mwake juma moja lililopita, wakidai ulikuwa na dosari na uonevu kwa mpinzani wake Jean Ping.

    Jumanne ya September 6 waangalizi wa umoja wa Ulaya walitoa tathmini ya ripoti ya waangalizi wake kwenye mji wa Haut-Ogooue, ambako ni ngome kuu ya Rais Bongo, ambapo wamesema kulikuwa na wizi mkubwa wa kura pamoja na kukiukwa kwa sheria na kanuni za uchaguzi.

    1 2 3 4 5 6 7 8
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako