• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii ( Septemba 3-Septemba 9)

    (GMT+08:00) 2016-09-09 19:50:28

    Obama akutana na rais wa Ufilipino baada ya sintofahamu

    Hatimaye Rais wa Marekani Barack Obama amekutana na mwenzake wa Ufilipino, Rodrigo Duterte nchini Laos baada ya rais huyu kumtusi kuwa ni "mwana wa kahaba". Awali mkutano kati ya marais hawa wawili ulifutiliwa mbali.

    Mzozo Kati ya Obama na Dulerte ulianza wakati Obama alibaini kwamba angemuuliza kiongozi Rais Rodrigo Dulerte maswali kuhusiana na mauaji ya kiholela ya watu wanaotuhumiwa kuhusika katika ulanguzi wa madawa ya kulevya nvchini Ufilipino.

    Kiongozi wa Ufilipino Rodrigo Duterte amesema hakukusudia kumtusi Rais Barack Obama na alisema anajutia kuona kwamba matamshi yake kumhusu kiongozi wa Marekani Barack Obama yamefasiriwa kama matusi.

    Bw Duterte alisema hayo baada ya Rais Barack Obama kufuta mkutano wake na kiongozi huyo kutokana na maneno ya lugha chafu yaliyoelekezwa kwake.

    Kiongozi huyo wa Ufilipino alikuwa amesema kwamba hatakubali kuulizwa maswali kuhusu ukiukwaji wa haki za kibinadamu nchini mwake.

    Alisema Ufilipino haitawaliwi na mtu yeyote baada ya kuwa koloni ya Marekani kabla ya Uhuru wake.

    1 2 3 4 5 6 7 8
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako