• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii ( Septemba 3-Septemba 9)

    (GMT+08:00) 2016-09-09 19:50:28

    IS yapoteza ngome kwenye mpaka wa Uturuki na Syria

    Waziri Mkuu wa Uturuki Binali Yildirim, wiki hii anasema kwamba mpaka wa Uturuki na Syria sasa uko salama kabisa na vikosi vya Uturuki vinadhibiti eneo hilo. Kundi la Islamic State limepoteza maeneo iliyokua ikiyashikilia hivi karibuni.

    Kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miaka miwili, kundi la Islamic State limepoteza ngome zake zote kwenye mpaka wa Uturuki na Syria.

    Mapigano mapya yaliyoanzishwa na jeshi la Uturuki katika eneo la Al-Ain yalizaa haraka matunda, kwani yalilazimisha wapiganaji wa kijihadi wa kundi la Islamic State kukimbilia katika eneo la kusini, na hivyo kupelekea Uturuki kudhibiti mpaka wake wa kusini na Syria, kuanzia eneo la Jarablos hadi Azaz.

    Pamoja na kushindwa kushindwa huko, kundi la Islamic State limepoteza mawasiliano yoyote na makundi mengine washirika yalioko maeneo tofauti duniani. Kupoteza eneo hili la mpakani, litapelekea kundi hili kushindwakuajiri wapiganaji wapya na kupata chakula na vifaa vingine kutoka Uturuki.

    1 2 3 4 5 6 7 8
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako