• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii ( Septemba 3-Septemba 9)

    (GMT+08:00) 2016-09-09 19:50:28

    Jaribio kubwa la nyuklia la Korea Kaskazin lasababisha tetemeko la ardhi

    Maafisa wa jeshi la Korea Kusini wamesema Korea Kaskazini imetekeleza jaribio la tano na kubwa zaidi la kifaa cha nyuklia Ijumaa.

    Rais wa Korea Kusini Park Geun-hye ametaja jaribio hilo kuwa "jaribio la kujiangamiza" ambalo linaonyesha "kutomakinika" kwa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.

    Maafisa wa Seoul wanasema mitambo yao iligundua tetemeko la ardhi ya nguvu ya 5.3 kwenye vipimo vya Richter karibu na eneo ambalo Pyongyang hutumia kufanya majaribio ya vifaa vya nyuklia.

    Hadi wakati tukienda hewani Korea Kaskazini haikuwa imesema lolote kuhusu jaribio hilo, lakini wachanganuzi wanasema hii huenda ikawa ishara ya hatua zilizopigwa na taifa hilo katika kustawisha teknolojia yake ya nyuklia.

    Bi Park, ambaye amesitisha ghafla ziara yake ng'ambo, amesema baada ya kutekeleza jaribio hilo la tano la nyuklia "serikali ya Kim Jong-un itakaribisha vikwazo zaidi na kutengwa zaidi na jamii ya kimataifa."

    Jaribio hilo linadaiwa kuzalisha nguvu ya kilotani 10, nguvu mara dufu ya jaribio lililotekelezwa Januari.


    1 2 3 4 5 6 7 8
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako