Timu ya wanawake ya kandanda ya Kenya Harambee Starlets imewaadhibu wenyeji Crested Cranes ya Uganda mabao 4-0 katika mechi yao ya ufunguzi ya Soka ya Afrika Mashariki ya Wanawake (Cecafa) mjini Jinja nchini Uganda, Jumapili.
Mabao hayo yalipatikana kupitia wachezaji Esse Akida, ambaye alifunga mawili, na Corazon Aquino na Mary Kinuthia waliocheka na nyavu mara moja kila mmoja.
Timu hiyo ya Starlets inanolewa na kocha David Ouma
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |