• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya kuvutia uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje wa dola bilioni 2

    (GMT+08:00) 2016-09-12 21:03:44

    Kenya iko mbioni kuvutia uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje wa dola za Kimarekani bilioni 2 mwaka huu.

    Waziri wa viwanda, biashara na misingi ya ushirikiano Julius Korir, amesema uwekezaji unatoka maeneo mbalimbali duniani, lakini vyanzo vikubwa vitakuwa China, India na Umoja wa Ulaya. Akiongea kwenye jukwaa la uhamasishaji wa vyombo vya habari la Benki ya Dunia, Korir amesema uwekezaji unaonesha kuwa mageuzi ya biashara ya Kenya yameanza kuzaa matunda. Kwa mujibu wa waziri huyo wawekezaji wa kigeni wanakwenda Kenya ili kuweza kutumia eneo la kimkakati la Kenya.

    Amefafanua akisema uwekezaji huo unamiminika kwenye viwanda vyote vikubwa, nguo, biashara ya kilimo, utalii pamoja na ukusanyaji wa vyombo vya usafiri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako