• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakimbiaji wa Ethiopia watawala mbio za marathon za Beijing 2016

    (GMT+08:00) 2016-09-17 18:41:35


    Wakimbiaji wa Ethiopia wametawala kwenye mbio za marathon za Beijing za mwaka 2016 na kuzoa medali zote tatu kwenye mbio za wanaume huku wanawake wakijizolea medali za dhahabu na fedha.

    Gebre Mekuant Ayenew, ameshinda medali ya dhahabu kwa kukimbia kwa muda wa saa 2:11:09. Mwenzake Dadi Feyera Gemeda amechukua nafasi ya pili kwa kukimbia kwa saa 2:11:30, akifuatiwa na Bekele Mesfin Teshome aliyeandikisha muda wa saa 2:11:56.

    Kwa upande wa wanawake, Muethiopia Biru Meseret Mengistu amerudi nyumbani na medali ya dhahabu kwa kukimbia kwa saa 2:25:56, rikodi ambayo ni bora zaidi kwa upande wa wanawake katika miaka 10 iliyopita. Naye Tola Melkam Gizaw wa Ethiopia na Jo Un Ok kutoka Korea Kaskazini wamechukua nafasi ya pili na tatu mtawalia.

    Mbio za marathon za Beijing, ambazo mwaka huu zimeingia kwenye toleo lake la 36, zilipokea maombi 66,576 lakini wakimbiaji elfu 30 tu ndio waliopata nafasi ya kushiriki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako