• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Rio 2016 yamalizika

    (GMT+08:00) 2016-09-19 20:10:08

    Michezo ya 15 ya Olimpiki ya Walemavu ya majira ya joto imemalizika jana usiku mjini Rio, Brazil.

    Katika siku 12 zilizopita, wanamichezo walemavu zaidi ya 4,400 kutoka nchi na sehemu 160 duniani walishiriki kwenye michezo hiyo. Wanamichezo kutoka China wamepata medali 239 zikiwemo 107 za dhahabu, na hivyo kuifanya China kuongoza kwa medali. Uingereza imechukua nafasi ya pili kwa kupata medali 64 za dhahabu, na Ukraine imekuwa ya tatu kwa kupata medali 41 za dhahabu.

    Mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki ya Rio Carlos Arthur Nuzman amesema, mji wa Rio umefanikiwa kuandaa Michezo ya Olimpiki na Michezo ya Olimpiki ya Walemavu, ambayo imeufanya mji huo uwe mji wa Olimpiki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako