• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China asema China inatarajia kuondoa kabisa umaskini ifikapo mwaka 2020

    (GMT+08:00) 2016-09-20 18:35:56

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ameendesha kongamano la Umoja wa Mataifa kuhusu suala la maendeleo endelevu lililofanyika jana alasiri kwenye makao makuu ya umoja huo mjini New York. Akihutubia kongamano hilo Bw. Li Keqiang alisema, China inatarajia kuondoa kabisa umaskini kwa mujibu wa vigezo vyake ifikapo mwaka 2020.

    Kwenye kongamano hilo lenye kaulimbiu ya "Malengo ya maendeleo endelevu: kufanya juhudi kwa pamoja kuibadili dunia yetu—Mapendekezo ya China", waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang alifafanua kwa kina mtizamo wa China kuhusu maendeleo endelevu, na kusisitiza umuhimu wa kutimiza maendeleo yanayoungana yenye uwazi na shirikishi.

    "Msingi wa maendeleo endelevu ni maendeleo, na jambo moja muhimu katika maendeleo ni ukuaji. Kwa sababu bila maendeleo na ukuaji, yoyote mengine yatakuwa ni maneno matupu. Lakini kwa upande mwingine, maendeleo ni lazima yawe endelevu, yawe na uratibu kwa pande za uchumi na jamii, ambapo binadamu na mazingira vinaishi kwa masikilizano, na vilevile yanatakiwa kuwa maendeleo yanayoungana na yenye uwazi na ushirikishi. Tunaweza kusema kutimiza maendeleo endelevu ni shughuli ya pamoja ya dunia nzima."

    Bw. Li Keqiang amesema, China imeanza kutekeleza kwa pande zote ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030, na imetoa mpango wake kutekeleza ajenda hiyo na kuuweka kwenye mkakati wa jumla wa maendeleo ya nchi. Bw. Li Keqiang amesema,

    "Tunatarajia kutimiza lengo la kuwasaidia watu wanaoishi chini ya vigezo vya umaskini vilivyowekwa na China waondokane kabisa na umaskini ifikapo mwaka 2020, na kufikia malengo kabla ya wakati katika maeneo ya kuondoa umaskini na njaa, afya ya watoto na wanawake na uhakikisho wa nyumba. Ifikapo mwaka 2030, China inatumai kuweza kukaribia kiwango cha nchi zilizoendelea."

    Mbali na mafanikio yanayokubalika duniani ikiwemo maendeleo ya kiuchumi, kuondoa umaskini na kuhimiza usawa wa kijinsia, kwa ngazi ya kikanda na kimataifa, pendekezo la Ukanda mmoja na Njia moja lililotolewa na serikali ya China pia linadhaniwa kuwa limesaidia nchi nyingine, haswa nchi zinazoendelea, kuimarisha ujenzi wa uwezo, kuinua viwango vya teknolojia na kuhimiza mchakato wa kurahisisha uwekezaji na biashara ya kimataifa, na hatimaye kusaidia kutimiza malengo ya maendeleo endelvu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako