• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kibarua cha kocha wa Valencia CF chaota mbawa

    (GMT+08:00) 2016-09-22 10:04:21
    Klabu ya Valencia CF imetangaza kumfukuza kazi meneja Pako Ayesteran kufuatia kufanya vibaya kwa kikosi hicho tangu walipoanza msimu wa 2016/17, ikiwa ni miezi sita tu tangu walipomtangaza kuwa mkuu wa benchi la ufundi badala ya Gary Neville aliyetimuliwa mwishoni mwa msimu uliopita.

    Valencia CF ipo mkiani mwa msimamo wa ligi ya Hispania La Liga na mpaka sasa hawajapata point yoyote katika michezo minne waliyocheza.

    Mwishoni mwa juma lililopita walipoteza kwa kufungwa mabao mawili kwa moja dhidi ya Athletic Bilbao, hatua ambayo iliongeza chachu kwa viongozi kuafiki maamuzi ya kumtimua meneja huyo kutoka nchini Hispania. Ayesteran anakua meneja wanane kutimuliwa na uongozi wa klabu hiyo, tangu mwaka 2012.

    Kufuatia maamuzi hayo, kocha wa kikosi cha wakubwa klabuni hapo Salvador Gonzalez (Voro) ameteuliwa kuwa meneja wa muda, hadi hapo uongozi wa Valancia CF utakapompata mkuu wa benchi la ufundi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako