• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rivatex kupanda pamba

    (GMT+08:00) 2016-09-22 20:33:13

    Kiwanda cha nguo nchini Kenya Rivatex kimepanga kupanda pamba katika ardhi ya ekari 500 ili kupanua uzalishaji wake. Kiwanda hicho ambacho kinamilikiwa na chuo kikuu cha Moi kinapania kupanda pamba hiyokatika eneo la Bura, Pwani kama njia moja ya kuongeza malighafi yake. Mkurugenzi wa kiwanda hicho Thomas Kipkurgat amesema licha ya kiwanda hicho kuwa na mitambo ya kisasa bado kinashuhudia uhaba wa malighafi. Amesema wana soko zuri la bidhaa za nguo lakini changamoto ni uhaba wa malighafi na kuwataka wakulima wa maeneo ya Nyanza na Magharibi kufufua kilimo cha pamba. Amesema mbali na kupanda pamba,kiwanda hicho pia kinashirikiana na wakulima kutoka eneo la Mogotio kupanda pamba katika shamba lingine la ekari 250 kupanua uzalishaji wa zao hilo.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako