• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Darubini kubwa kabisa duniani ya kuchunguza sayari na nyota yaanza kufanya kazi

    (GMT+08:00) 2016-09-25 16:47:55

    Darubini kubwa zaidi duniani ya kuchunguza sayari na nyota imeanza kufanya kazi hii leo katika mkoa wa Guizhou ulioko kusini magharibi mwa China.

    Leo mchana, mamia ya wanaanga na mashabiki wa mambo ya anga walishuhudia kuanza rasmi jukumu la darubini hiyo la kuchunguza anga ya juu na kutafuta kama kuna maisha katika anga hiyo.

    Mradi wa ujenzi wa darubini hiyo uliogharimu dola za kimarekani milioni 180 ulianza mwaka 2011, ikiwa ni miaka 17 baada ya kupendekezwa na wanaanga wa China.

    Rais Xi Jinping wa China ametuma barua ya pongezi kwa wanasayansi, wahandisi, na wajenzi wa darubini hiyo mara ilipoanza rasmi kufanya kazi hii leo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako