• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Usalama lasikitishwa kwa kucheleweshwa tena uchaguzi wa bunge na urais nchini Somalia

    (GMT+08:00) 2016-09-29 16:29:08

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeeleza kusikitishwa na kucheleweshwa tena kwa uchaguzi wa bunge na rais nchini Somalia, na kuzitaka pande zote za Somalia kufuata ratiba mpya na kufikia haraka makubaliano juu ya changamoto za kisiasa.

    Kwenye taarifa yao, nchi 15 wajumbe wa baraza hilo wamesisitiza kuwa kufanya uchaguzi wa amani, uwazi na jumuishi itakuwa ni hatua ya kihistoria kwa Wasomali wote, na pia ni msingi wa nchi hiyo katika kupata maendeleo ya kuelekea kwenye demokrasia na utulivu.

    Uamuzi wa kuahirisha uchaguzi ni mara ya pili kutolewa na Tume ya uchaguzi ya Somalia tangu mwezi Agosti, ambao chaguzi zote mbili zilipangwa kufanyika wakati huo. Sasa tume hiyo imepanga uchaguzi wa bunge kufanyika Oktoba 23 hadi Novemba 10, na ule wa rais Novemba 30.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako