• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maonesho ya biashara ya Guangzhou yatahimiza maboresho ya biashara ya China na nje

    (GMT+08:00) 2016-09-29 16:47:57

    Wizara ya biashara ya China imesema, Maonesho ya 120 ya biashara ya Guangzhou, China yatakayofanyika kuanzia mwezi Oktoba hadi Novemba yatasaidia kuimarisha maendeleo na kuhimiza maboresho ya biashara ya China na nchi za nje.

    Akitoa tathmini ya maonyesho hayo katika ukuaji wa biashara na nje nchini China, msaidizi wa waziri wa biashara wa China Zhang Ji amesema, kila mwaka maonesho hayo yanavutia wafanyabiashara karibu laki 4 kutoka nchi na sehemu zaidi ya 210 duniani, ambayo inachangia maingiliano ya uchumi na biashara na mawasiliano ya utamaduni kati ya China na nchi za nje.

    Naye mkurugenzi wa Kituo cha biashara na nje cha China Li Jinqi amesema, hivi sasa biashara na nje ya China inakabiliwa na changamoto kubwa, hata hivyo Maonesho ya biashara ya Guangzhou yakiwa jukwaa muhimi la kuhimiza biashara na nje, yatachukua hatua mbalimbali zinazolenga kuinua kiwango cha utaalamu na kimataifa cha maonesho hayo, ili kuzisaidia kampuni za China zinazofanya biashara na nchi za nje kubadilisha njia yao ya kujiendeleza, kupanua soko nje ya China, na kupata nguvu bora mpya katika ushindani wa kibiashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako