• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya kuanza kutumia mfumo mpya wa ujenzi

    (GMT+08:00) 2016-09-29 21:08:51

    Katibu Mkuu katika Wizara ya Ujenzi nchini Kenya Profesa Paul Maringa amesema kuwa hivi karibuni Kenya itaanza kutekeleza mfumo mpya wa ujenzi kwa sababu mfumo wa zamani umepitwa na wakati.

    Kanuni mpya za ujenzi zinazofahamika kama Eurocodes zinatarajiwa kutoa nafasi ya matumizi ya teknolojia mpya na nyenzo asilia za ujenzi.

    Wajenzi nchini Kenya wamekuwa wakitumia mfumo wa Uingereza,lakini Uingereza iliacha kutumia mfumo huo baada ya kutekeleza mfumo mpya wa Eurocodes mwaka 2010.

    Aidha Mkurugenzi wa Shirika la Kitaifa la kutathmini ubora wa bidhaa (Kebs) Bw Charles Ongwae amesema wasikadau katika sekta ya ujenzi wana muda wa miaka mitano kuanza kutekeleza mfumo huo mpya kutoka mwaka huu hadi mwak 2021.

    Ongwae amesema kanuni mpya za ujenzi zitazingatia mambo mengi kama vile usafi,hewa safi,uwezo wa kukabiliana na moto,miongoni mwa mambo mengine yanayoimarisha usalama wa wakazi.

    Kulingana na Ongwae ,kutekelezwa kwa kanuni mpya kunalenga kurahisisha biashara kutokana na kuwa Kenya itakuwa mwanachama wa kundi kubwa la mataifa ambayo yanatumia kanuni hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako