• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  •  KRC Genk yaibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Sassuolo 

    (GMT+08:00) 2016-09-30 09:42:05
    Jana usiku klabu ya KRC Genk inayochezewa na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Mbwana Samatta ilishuka uwanjani kucheza mchezo wake wa pili wa Kundi F wa ligi ya Europa dhidi ya Sassuolo ya Italia, Genk waliwakaribisha Sassuolo katika uwanja wao wa nyumbani wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa mchezo wao wa kwanza dhidi ya Rapid Wien.

    Mchezo huo ulimalizika kwa KRC Genk kuibuka na ushindi mnono wa magoli 3-1, magoli ambayo yalifungwa na Nikolaos Karelis dakika ya 8, mjamaica Leon Bailey dakika ya 25 na Thomas Buffel dakika ya 61 wakati goli la Sassuolo lilifungwa na Matteo Politano dakika ya 65.

    Mtanzania Mbwana Samatta ambaye alikuwa majeruhi aliingia dakika ya 75 kuchukua nafasi ya mgiriki Nikolaos Karelis , ushindi huo wa KRC Genk unakuja ikiwa ni baada ya kukubali kipigo cha magoli 3-2 katika mchezo wa kwanza ugenini dhidi ya Rapid Wien, Genk sasa watacheza mchezo wao wa tatu October 20 dhidi ya Athletic Bilbao ya Hispania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako