• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yakosa kuandaa michuano ya Rollball Afrika

    (GMT+08:00) 2016-09-30 09:42:28
    Chama cha mchezo wa Rollball nchini Tanzania TRBA kimesema kinajipanga vyema kwa ajili ya kuandaa mashindano ya Afrika Mashariki mara baada ya kukosa nafasi ya kuandaa mashindano ya Afrika ambayo rasmi yatafanyika nchini Uganda Mei mwakani.

    Rais wa TRBA, Noel Kihunsi amesema, wataitumia fursa waliyoipata ili kuhakikisha wanawavuta vijana wengi zaidi waweze kuuelewa na kushiriki katika mchezo huo ikiwa ni pamoja na kupata vijana wengi watakaoiwakilisha nchi katika mashindano ya Kombe la Dunia yatakayofanyika Desemba mwakani nchini Uganda. Kihunsi amesema, kwa sasa pia wapo katika maandalizi ya mashindano ya taifa ambapo wanaendelea kufuatilia taratibu zinazotakiwa katika kuandaa mashindano hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako