• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kipchoge Keino kuendelea na wadhifa wake kwenye NOCK

    (GMT+08:00) 2016-09-30 09:42:51
    Mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki ya Kenya (NOCK) Dkt Kipchoge Keino sasa yuko huru kuendelea na wadhifa wake hadi uchaguzi utakapofanywa baada ya jana marufuku yake kuondolewa.

    Kamati ya muda iliyoundwa na Waziri wa Michezo, Dkt Hassan Wario baada ya kuivunja NOCK kwa sababu ya sakata la Olimpiki la mwaka 2016 mwezi Agosti, imesema marufuku ya Keino iliyoanza Septemba 10 imesitishwa ili maandalizi ya uchaguzi yaanze.

    Katika barua iliyoandikwa na katibu mkuu wa kamati hiyo ya muda Andrew Mudibo, vyama vilivyoko chini ya NOCK vilikubaliana kuwa lazima NOCK ichague viongozi wapya kabla ya Desemba 31 mwaka 2016. Kamati ya Kioni imetoa ratiba itakayofuatwa kabla ya uchaguzi huo kufanywa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako