• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNHCR yarejesha wakimbizi zaidi ya 30,000 wa Somalia kutoka Kenya

    (GMT+08:00) 2016-09-30 13:04:09

    Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limesema kuanzia mwezi Desemba mwaka 2014 wakimbizi zaidi ya elfu 30 wa Somalia wamerejeshwa kwao kwa hiari kutoka kambi ya wakimbizi ya Dadaab iliyoko magharibi kaskazini mwa Kenya.

    Shirika hilo limesema katika kipindi cha ripoti hiyo kuanzia tarehe 1 hadi 15 mwezi Septemba, wakimbizi 482 wamerejeshwa Somalia kwa ndege.

    Kwa sasa Kenya inashirikiana na UNHCR katika mradi utakaohakikisha kurejeshwa kwa utaratibu na hiari kwa wakimbizi 50,000 wa Somalia kutoka kambi ya wakimbizi ya Dadaab, ambayo serikali ya Kenya ilitangaza kuifunga mapema mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako