• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkurugenzi wa IMF asema China ni mchangiaji mkuu wa ukuaji wa uchumi wa dunia

    (GMT+08:00) 2016-09-30 13:04:34

    Mkurugenzi wa IMF Bibi Christine Lagarde amesema nchi zinazoendelea ni nguvu kuu ya kuhimiza ongezeko la uchumi wa dunia na China yenye utendaji mzuri wa kiuchumi ni mchangiaji mkuu.

    Bibi Lagarde alipohudhuria shughuli ya shule moja ya biashara nchini Marakani alisema ingawa uchumi wa Marekani unakabiliwa na changamoto kadhaa, na mwaka huu IMF imepunguza mara kadhaa makadirio kuhusu ongezeko la uchumi wa Marekani.

    Bibi Lagarde pia amesema wakati China inafanya marekebisho ya miundo ya uchumi, bado inadumisha ongezeko la kasi la uchumi.

    Vielvile Bibi Lagarde amesisitiza umuhimu wa kupinga kujilinda kibiashara. Amezitaka nchi mbalimbali zifanye mageuzi ya miundo ya uchumi kwa mujibu wa umaalumu wao, kuratibu sera zao na kutimiza ongezeko la uchumi linaloshirikisha sekta mbalimbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako