• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Raul Castro akutana na viongozi wa Afrika kuimarisha ushirikiano wa kisiasa

    (GMT+08:00) 2016-09-30 18:44:26

    Rais wa Cuba Raul Castro jana alikutana na viongozi wa Lesotho na Namibia ili kusukuma mbele uhusiano na ushirikiano na nchi za Afrika.

    Kwa mujibu wa taarifa ya serikali ya nchi hiyo, Rais Castro alipokutana na waziri mkuu wa Lesotho Bw Pakalitha Bethuel Mosisili walibadilishana maoni kuhusu uhusiano kati ya pande mbili, na kueleza nia yao ya kuimarisha ushirikiano zaidi katika maeneo ya afya, elimu na michezo. Katika ziara yake nchini Cuba Mosisili alisaini makubaliano kadhaa ya ushirikiano.

    Rais Castro pia alikuwa na mazungumzo na rais wa kwanza wa Namibia na mwanaharakati mpinga ubaguzi wa rangi, Sam Nujoma ambaye pia amezuru nchini humo kuimarisha ushirikiano kati ya nchi mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako