• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Obama na Bibi Merkel wazilaani Russia na Syria kwa mashambulizi

    (GMT+08:00) 2016-09-30 18:44:58

    Rais Barack Obama wa Marekani na Chansela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel wamelaani mashambulizi yanayofanywa na Russia na Serikali ya Syria kaskazini mwa mji wa Allepo.

    Viongozi hao wanaamini kuwa Russia na serikali ya Syria wanawajibika na kukomesha mapigano nchini Syria na kutoa nafasi ya kupita kwa misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa kwenye maeneo yaliyozingirwa na yale ambayo ni magumu kupitika.

    Naibu mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Syria Bw Ezzeldin Ramzy amesema mashambulizi makali kaskazini mwa Allepo na magharibi mwa mji huo yanatishia maisha ya raia na kukwamisha ufikishaji wa misaada muhimu.

    Septemba 10, Russia na Marekani zilitangaza makubaliano ya kusimamisha vita katika nchi nzima, na pande zote mbili kutarajia kuwa makubaliano hayo yatasaidia kukomesha umwagaji damu wa miaka mitano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako