• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Masomo ya kidijitali kuwafaidi wakazi pia.

    (GMT+08:00) 2016-09-30 18:52:15

    Kutokana na mradi wa kueneza mafunzo ya kiteknolojia katika shule za umma, serikali imekuwa ikisamabaza umemem katika shule hizi na haswa zilizo mashianani. Kutokana na mpango huu wa usambazaji umeme, wakazi wengi huenda wakanufaika zaidi kwa kupata umeme.

    Akizungumza jijini Nairobi wakati wa uzinduzi rasmi wa mradi huu wa masomo ya dijitali, Waziri wa Nishati Bw, Charles Keter alisema kwamba tayari asilimia 95 ya vifaa vya kusambaza umeme vimenunuliwa na kazi rasmi itang'oa nanga juma lijalo. Waziri alisisitiza kwamaba umeme utasambazwa kwa shule zote nchini na maeneo yaliyo karibu.

    Kulingana na waziri, shule nyingi zimeanza kunufaika na mradi huu na zilizosalia ni shule chini ya 500, zitakazoshughulikiwa kuanzia juma lijalo.

    Baadhi ya shule zenye miundombinu inayofaa au zilizopo karibu na miji zilizounganishwa kweney mfumo wa taifa wa umeme ilhali nyinginezo hasa za mashinani zitawekewa vifaa vya kuzalkisha nguvu za umeme kwa kutumia miale ya jua.

    Jamii za mashinani zinatarajiwa kupigwa jeki zaidi na kunawiri kutokana na maendeleo yatakayochochewana mradi huu. Umeme huo pia utapanua fursa kwa wakazi na wajasiriamali wadogo watakaotegemea umeme huo kuendesha biashara zao.

    Wakati uo huo, wakazi wa mashinani watapata fursa ya kuunganishwa na mtandao bora wa intaneti kupitia mradi utakaogharimu zaidi ya shilingi milioni 400, kutoka Marekani.

    Shirika la The Overseas Private Investment Corporation (OPIC) likishirikiana na idara ya maendeleo nchini Marekani, tayari limetoa fungu la kwanza la mkopo huo na kuwakabidhi Mawingu Networks ; kampuni inayosimamia shughuli ya kuezeka vifaa vya kunasa miale ya jua na kuunganisha intaneti isiyotumia waya mashinani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako