• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Kiwanda cha nafaka, mafuta ya alizeti kujengwa dodoma.

    (GMT+08:00) 2016-09-30 18:53:56

    Huenda ukawa mwamko mwema kwa wakazi wa Dodoma Tanzania, baada ya mikakati ya kujenga kiwanda cha kusagisha nafaka na kukamua mafuta ya alizeti kupendekezwa kijengwe huko. Endapo hili litatimia, basi takriban watu 250 watanufaika kwa ajira kwenye kiwanda hicho.

    Mkurugenzi mkuu wa wa shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), profesa Godius Kahyarara alitoa ahadi hii alipokabidhi hundi ya shilingi bilioni 3.7 kwa mkurugenzi wa Bodi ya Nafaka na mazao Mchanganyiko, John Maige, yenye lengo la kununua mashine za usagaji wa nafaka na ile ya kukamulia mafuta ya alizeti.

    Profesa Kahyarara alisema kwamba utoaji wa fedha hizo, unaenda sambamba na sera ya uwekezaji ya NSSF ya kuwekeza michango ya wanachama wake kwenye miradi yenye faida.

    Naye mkurugenzi wa Bodi ya Nafaka na mazao mchanganyiko Bw. Maige amesema Bodi ya Nafaka na mazao mchanyiko kwa ushirikiano na NSSF, itatekeleza mradi huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako