• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kituo kikubwa cha kuzalisha umeme wa jua Afrika Mashariki chaanza kujengwa nchini Kenya

    (GMT+08:00) 2016-09-30 18:58:26

    Ujenzi wa kituo kikubwa zaidi cha kuzalisha umeme kwa nishati ya jua katika kanda ya Afrika Mashariki umeanza rasmi Garissa, Kenya.

    Kituo hicho kinachojengwa na kampuni moja ya China kinatarajiwa kuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 50 za umeme kwa mwaka ambao unaweza kukidhi mahitaji ya watu laki 3.5, nusu ya idadi ya jumla ya eneo la Garissa.

    Waziri wa nishati wa Kenya Bw Charles Keter amesema mradi huo unatarajiwa kuongeza uwezo wa Kenya kuzalisha na kusambaza umeme, na kupata watu wenye ustadi wa hali ya juu wa kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme kwa nishati ya jua.

    Akiongea kwenye uzinduzi wa ujenzi wa kituo hicho mjini Nairobi, balozi wa China nchini Kenya Bw. Liu Xianfa amesema mradi huo ni hatua iliyopigwa na China na Kenya katika ushirikiano wa teknolojia ya ngazi ya juu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako