• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki kuu ya China yasema uchumi wa China ni imara

    (GMT+08:00) 2016-10-07 20:54:33

    Benki kuu ya China imesema uchumi wa China kwa sasa unaendelea katika kasi yenye utulivu zaidi kuliko mwaka jana.

    Naibu Mkurugenzi wa Benki hiyo Bw Yi Gang amesema uchumi wa China unakua kwa kasi ya kati ya asilimia 6.5 na asilimia 7, na kuna hatua madhubuti za kupunguza ukosefu wa ajira na kupunguza mfumuko wa bei, ikiwa ni pamoja na kuongeza uzalishaji na kuboresha faida.

    Bw Yi amesema kuanzia mwaka jana, matumizi ya ndani yamekuwa ikichangia asilimia 70 ya pato la taifa la China, na kusema serikali itatumia zaidi hatua za kifedha na sera za kimuundo kufanya uchumi utegemee zaidi matumizi.

    Benki hiyo pia imesema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, China ilichangia asilimia kati ya 25 na 30 ya ongezeko la uchumi wa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako