• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shirikisho la Soka Hispania lafafanua kuhusu jezi ya Gerard Pique

    (GMT+08:00) 2016-10-11 09:25:35
    Mchezaji wa klabu ya Barcelona, Gerard Pique ametangaza kuwa msimamo wake bado upo pale pale kuwa atastaafu kuichezea timu ya Taifa ya Hispania baada ya michuano ya kombe la Dunia 2018, Russia. Beki huyo ameyasema hayo baada ya ushindi wa 2-0 ugenini dhidi ya Albania, mechi ambayo ilifanya mchezaji huyo kukosolewa sana kufuatia jezi aliyoivaa. Pique alivaa jezi ambayo mikononi ilikuwa haina mistari ya rangi ya bendera ya Hispania na hivyo kupingwa na kushambuliwa na mashabiki wengi hasa katika mitandao ya kijamii

    Mashabiki mara nyingi wamekuwa wakimzomea mchezaji huyo kufuatia kusapoti harakati za jimbo la Catalunya ambalo limekuwa likipigania uhuru wake kutoka Hispania. Hata Hivyo shirikisho la mpira wa miguu la Hispania "RFEF" lilitoa ufanunuzi juu ya jezi ya Pique kuwa mistari ya rangi ya bendera katika jezi za Adidas ipo kwa wanaotumia jezi za mikono mifupi na sio za mikono mirefu, hilo linathibitika katika jezi aliyovaa Sergio Ramos ya mikono mirefu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako