• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rajbir Rai atangaza kustaafu mbio za magari

    (GMT+08:00) 2016-10-11 09:26:01
    Baada ya kumaliza mbio za magari za Eldoret akiwa katika nafasi ya tatu, dereva shupavu Rajbir Rai amebainisha kuwa anapanga kustaafu mwishoni mwa msimu wa 2016. Rajbir, 26, alisema ametosheka na misimu mitano ambayo ameshiriki.

    Mbali na kuwika nchini Uganda, pia alinyakua mataji ya Kisumu na Eldama Ravine. Rajbir alianza taaluma ya mbio za magari akiendesha vigari katika uwanja wa Jamhuri Park kabla ya kushiriki mbio za kwanza za magari katika Safari Rally mwaka 2012 katika kitengo cha 2WD, na mwaka 2013 alijitosa katika kitengo cha KNRC. Katika duru ya Eldoret Rally iliyoandaliwa Oktoba 8 katika kaunti za Uasin Gishu na Elgeyo-Marakwet, Rajbir alimaliza katika nafasi ya tatu akiendesha Ford Fiesta. Duru ya mwisho ya Mbio za Magari za Kitaifa (KNRC) msimu 2016 ya Guru Nanak itaandaliwa Novemba 26-27.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako