• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapinga shutuma za shirika lisilo la kiserikali la Marekani dhidi ya walinzi wa amani wa China nchini Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2016-10-11 18:55:29

    Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya China Yang Yujun amesema askari wa kulinda amani wa China nchini Sudan Kusini walijitahidi kudhibiti hali na kuwatuliza raia waliokuwa na hofu, kufuatia agizo la Umoja wa Mataifa katika mapigano makali yaliyotokea katikati ya mwezi Julai huko Juba, mji mkuu wa nchi hiyo.

    Yang amesema hayo baada ya shirika lisilo la kiserikali la Marekani "Kituo cha Raia Kwenye Mapigano" hivi karibuni kutoa ripoti ikivishutumu vikosi vya Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS wakiwemo askari wa China kushindwa kukabiliana na mapigano hayo. Yang anasema shutuma hizo hazilingani na hali halisi.

    "Mwezi Julai mwaka huu wakati mapigano yalipoibuka nchini Sudan Kusini, askari wa kulinda amani wa China walifuata agizo la UNMISS na kutekeleza jukumu la kulinda usalama wa makao makuu ya UNMISS mjini Juba na kambi ya wakimbizi No. 1 iliyo karibu. Wakati mapigano yalipozidi kuwa makali, askari wa China walishikilia nafasi zao na kutekeleza majukumu yaliyotolewa na UNMISS baada ya gari lao moja kushambuliwa na roketi na kuua wenzao wawili na wengine watano kujeruhiwa."

    Ameongeza kuwa hivi sasa Umoja wa Mataifa unafanya uchunguzi kuhusu jinsi UNMISS ilivyokabiliana na mapigano hayo, na kabla ya matokeo rasmi kutolewa, shutuma yoyote dhidi ya operesheni ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa na walinzi wa amani haina msingi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako