• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yapangiwa tena kundi gumu kwenye michuano ya raga ya Dubai Sevens

    (GMT+08:00) 2016-10-12 09:43:17
    Kenya itafungua Raga za Dunia za 2016-2017 dhidi ya Ufaransa katika duru ya ufunguzi ya Dubai Sevens mnamo Desemba 2. Katika ratiba iliyotangazwa na Shirikisho la Raga duniani (World Rugby) Jumatatu, Ikiwa kundi D Shujaa italimana na Les Bleus mnamo Desemba 2. Baadaye Kenya itakabiliana na Japan na Australia katika siku hiyohiyo. Kundi iliyopangiwa Kenya linaonekana kuwa gumu, kwani iliwahi kukutana na Ufaransa, Australia na Japan katika Dubai Sevens katika Raga za Dunia za msimu 2015-2016, na kupigwa 14-12 na Australia katika mechi za makundi na pia ililimwa 33-7 na Ufaransa katika mechi ya nusu-fainali ya Sahani.

    Kenya iliishinda Japan 17-12 katika mechi ya robo-fainali kabla ya kukutana na Ufaransa katika nusu-fainali. Kenya ililemewa na Australia na Ufaransa msimu wote uliopita. Ilimaliza katika nafasi ya saba nazo Australia na Ufaransa zilimaliza katika nafasi ya nne na 11, mtawalia. Japan inarudi kushiriki duru zote 10 za Raga za Dunia baada ya kuwa nje msimu mmoja. Dubai Sevens itakamilika Desemba 3, 2016.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako