• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2017 zazinduliwa jijini Dar es Salaam

    (GMT+08:00) 2016-10-14 10:08:55
    Mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2017 ambazo ni za 15 tangu Kuanzishwa kwake, zimezinduliwa rasmi jana jijini Dar es Salaam katika mkutano na wanahabari, wadhamini na Chama Cha Riadha Tanzania.

    Akizungumzia matunda ya udhamini wao Mkurugenzi wa Masoko wa TBL Group, Kushilla Thomas. alisema mwaka huu wameshuhudia mshiriki wa Kili Marathon akishiriki katika michezo ya Olimpiki ya Brazil na kumaliza katika nafasi ya tano katika mbio za kilomita 42.

    Kwa upande wake, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli ametaja zawadi kwa mbio za km 42 Kilimanjaro Premium Lager Marathon ni pamoja na – jumla ya Tsh milioni 20 kwa washindani wanaume na wanawake watakaoshika nafasi 10 za juu. Mshindi wa kwanza kutoka kila kundi atapata Tsh milioni 4 kila mmoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako