• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Iraq laanza operesheni kubwa ya kutwaa tena mji wa Mosul kutoka kwa kundi la IS

    (GMT+08:00) 2016-10-17 17:59:55

    Waziri mkuu wa Iraq Bw Haider al-Abadi ametangaza kuanza kwa operesheni kubwa ya kutwaa tena udhibiti wa mji wa pili kwa ukubwa nchini Iraq Mosul kutoka kwa kundi la IS.

    Bw Abadi ametoa taarifa kupitia televisheni ya taifa ya Al Iraqiya akisema operesheni ya kuukomboa mkoa wa Nineveh imeanza, na wakati wa ushindi umefika.

    Kwenye televisheni, Bw Abadi ambaye pia ni kamanda mkuu wa jeshi la Iraq alionekana amevalia sare za jeshi akiwa pamoja na maofisa wa ngazi ya juu wa jeshi.

    Bw Abadi ameahidi kuujenga upya mji wa Mosul, wilaya na vijiji vingine mkoani Nineveh baada ya kuharibiwa na wapiganaji wa kundi la IS.

    Habari kutoka idara ya usalama ya Iraq zinasema, kikosi cha usalama cha Iraq kimetwaa tena vijiji 9 kutoka kwa wapiganaji wa kundi la IS.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako