• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanaanga kwenye chombo cha anga ya juu cha China waonekana kuwa katika afya nzuri

    (GMT+08:00) 2016-10-20 20:51:26

    Upimaji wa afya kutoka mbali umeonesha kuwa wanaanga wawili walioko kwenye kituo cha anga ya juu cha China Tiangong-2 wanaonekana kuwa kwenye afya nzuri.

    Wakisaidiwa na mfumo uliotengenezwa na China unaounganisha maabara ya anga ya juu na kituo cha uongozi wa safari za anga za juu kilichoko ardhini, madaktari walio duniani wamefanya upimaji wa mara kwa mara na kuona wanaanga hao wako kwenye hali nzuri.

    Wanaanga hao Jing Haipeng na Chen Dong wako kwenye safari ya chombo cha anga ya juu chenye binadamu, jana waliondoka kwenye chombo cha Shenzhou 11 na kuingia kwenye maabara ya Tiangong 2, wataishi kwenye maabara hiyo kwa siku 30 kabla ya kurudi duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako