• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • David Moyes akalia kuti kavu klabuni kwake Sunderland

    (GMT+08:00) 2016-10-21 09:09:07

    Mkosi wa kutemwa umeanza tena kumuandama kocha David Moyes. Moyes, ambaye alijiunga na Sunderland mnamo Julai 23 mwaka 2016, anaongoza orodha ya makocha katika Ligi Kuu ya Soka ya Uingereza wanaokabiliwa na hatari ya kutemwa kabla ya msimu 2016-2017 kukamilika.

    Kulingana na gazeti la Daily Star, Moyes ambaye alifurushwa na Manchester United mnamo Aprili 22 mwaka 2014 na kutimuliwa tena na Real Sociedad mnamo Novemba 9 mwaka 2015, sasa uwezekano wa MScotland huyo kutimuliwa ni asilimia 91. Gazeti hilo linadai mechi kati ya Sunderland na West Ham United itakayochezwa kesho inaweza kuwa ya mwisho kwa Moyes ikiwa Sunderland itabwagwa.

    Sunderland ndiyo timu pekee katika Ligi Kuu ya Uingereza yenye jumla ya klabu 20, ambayo haijapata ushindi msimu huu. Inaburura mkia.

    Makocha wengine waliokalia kuti kavu ni Tony Pulis wa West Bromwich Albion, Aitor Karanka wa Middlesbrough, Slaven Bilic wa West Ham na Antonio Conte wa Chelsea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako