• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maadhimisho ya miaka 80 ya ushindi wa safari ya masafa marefu yafanyika

    (GMT+08:00) 2016-10-21 11:21:53

    Maadhimisho ya miaka 80 ya ushindi wa safari ya masafa marefu ya jeshi la chama cha kikomunisti cha China CPC yamefanyika leo asubuhi hapa Beijing.

    Safari ya masafa marefu ni uhamaji wa kijeshi na kimkakati uliofanywa jeshi la CPC kati ya mwaka 1934 hadi 1936.

    Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa chama cha kikomunisti cha China ametoa hotuba kwenye maadhimisho hayo akisema kupigania maendeleo ya taifa ni kama safari ya masafa marefu katika zama mpya.

    Mwezi Oktoba mwaka 1934, jeshi la chama cha kikomunisti cha China lililazimishwa kuhama kutoka kwenye makao makuu yake ili kukwepa kuzingirwa na jeshi la chama cha Kuomintang cha China, na kuanza safari ya masafa marefu yenye umbali wa zaidi ya kilomita elfu 12.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako