• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Iraq ladhibiti tena mji wa Hamdaniyah kutoka IS

    (GMT+08:00) 2016-10-22 17:08:53

    Vikosi vya usalama vya Iraq vimeukomboa mji wa Hamdaniyah kutoka kwa wapiganaji wa kundi la IS karibu na mji wa Mosul huku mashambulizi makali yakiendelea kwa lengo la kukomboa maeneo mengi zaidi kwenye mji huu.

    Duru za kijeshi zinasema vikosi hivyo vilipandisha bendera ya taifa la Iraq kwenye jengo la serikali ya huko katikati ya Hamdaniyah, na pia kudhibiti kijiji cha karibu cha kikristo cha Karamlis baada ya wapiganaji wa IS kukimbia kambi zao.

    Mapambano makali yanaendelea katika sehemu ijulikanayo kama Ninebeh Plain, ambayo iko mashariki na kaskazini mashariki mwa Mosul, mji mkuu wa mkoa wa kaskazini wa Nineveh, nchini Iraq.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako