• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Real Madrid yaibuka kidedea dhidi ya Athletic Bilbao, huku Ronaldo akiwa na siku 38 bila kupata goli

    (GMT+08:00) 2016-10-24 10:09:22
    Siku ya jana kulikuwa na michezo mingi ya Ligi Kuu mbalimbali barani Ulaya, na mchezo kati ya Real Madrid dhidi ya Athletic Bilbao ulikuwa ni moja kati ya michezo ya kuvutia iliyochezwa usiku wa Jumapili ya October 23. Real Madrid walishuka dimbani kuwakaribisha Athletic Bilbao kucheza mchezo wao wa 9 wa Ligi Kuu Hispania, ikiwa nyota wao Cristiano Ronaldo aliingia katika mchezo huo akiwa na kumbukumbu ya mara ya mwisho kufunga goli katika uwanja wa Santiago Bernabeu September 14 2016, sawa na siku 38 bila goli na hicho ndio kipindi chake kirefu kuwahi kukaa bila kufunga goli Bernabeu toka ajiunge na timu hiyo. Real Madrid walifanikiwa kuzibakisha point zote tatu nyumbani kwa kuifunga Athletic Bilbao magoli 2-1, Real Madrid walipata goli la kwanza dakika ya 7 kupitia kwa Karim Benzema ila Bilbao wakasawazisha dakika ya 27 kupitia kwa Sabin Merino, mchezo ulizidi kuwa mgumu na Real Madrid walilazimika kusubiri hadi dakika ya 83 Alvaro Morata alifunga goli la ushindi.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako