• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Julius Chepkwony Rotich na Priscah Jepleting Cherono wazoa medali za dhahabu kwenye Marathon ya Venice

    (GMT+08:00) 2016-10-24 10:10:20
    Wakenya Julius Chepkwony Rotich na Priscah Jepleting Cherono Jana waliibuka washindi wa mbio za 31 za Marathon ya Venice kwa mwaka wa pili mfululizo nchini Italia.

    Bingwa wa mwaka jana Rotich alitwaa taji lake kwa kutumia saa 2:10.

    Rotich, 28, ambaye alishinda taji la Marathon ya Geneva nchini Uswizi mnamo Mei 8 mwaka huu, aliongoza Wakenya Titus Masai na Francis Maina Ngare kufagia nafasi tatu za kwanza.

    Kwa upande wa Cherono, 36, na Mkenya mwenzake Ester Wanjiru Macharia walinyakua nafasi mbili za kwanza katika kitengo cha kinadada. Bingwa mara tatu wa marathon nchini Italia, Ivana Iozzia alikamata nafasi ya tatu. Cherono alikamilisha umbali wa kilomita 42 kwa saa 2:27, ni Mkenya wa kwanza kushinda mbio hizi tangu Mercy Kibarus mwaka 2013.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako