Gazeti la Chama cha Kikomunisti cha China People's Daily limeikosoa Marekani kwa kuruhusu meli yake ya kivita kuingia kwenye eneo la bahari la China katika Bahari ya Kusini ya China, na kusema vitendo kama hivyo vitaongeza kushuka kwa ushawishi wa Marekani.
Makala iliyochapishwa kwenye gazeti hilo imesema, meli hiyo ya Marekani iliingia kwenye eneo la bahari la China karibu na visiwa vya Xisha ijumaa iliyopita.
Makala hiyo imesema, hatua hiyo ya meli ya Marekani ni ukiukwaji mkubwa wa haki na mamlaka ya China na sheria za kimataifa, na kwamba hatua hiyo pia imevuruga amani, usalama, na utaratibu katika eneo hilo la bahari.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |