• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Guinea kufanya ziara nchini China

    (GMT+08:00) 2016-10-24 18:52:22

    Rais Alpha Conde wa Guinea atafanya ziara nchini China kuanzia tarehe 26 mwezi huu hadi tarehe 4 mwezi ujao.

    Katika ziara hiyo, rais Conde atakutana na mwenyeji wake rais Xi Jinping, waziri mkuu Bw. Li Keqiang pamoja na spika wa bunge la umma la China Zhang Dejiang.

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Lu Kang amesema uhusiano kati ya China na Guinea ni mzuri na wa kihistoria, na katika miaka ya hivi karibuni, ushirikiano kati ya nchi hizo umeendelezwa kwa kasi kwenye sekta mbalimbali, na inaaminika kuwa ziara hiyo itainua uhusiano kati ya nchi hizo mbili ufikie ngazi ya juu zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako