• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maharamia wa Somalia wawaachia huru mateka 26 waliowashikilia kwa miaka mitano

    (GMT+08:00) 2016-10-24 19:58:44
    Shirika la kimataifa la safari za majini Oceans Beyond Piracy limesema, Jumamosi iliyopita maharamia wa Somalia waliwaachia huru watu 26 waliowashikilia kwa karibu miaka mitano.

    Mratibu wa kikanda wa shirika hilo Bw. John Steed amesema meli moja ya uvuvi yenye bendera ya Oman NAHAM 3 ilitekwa nyara kusini mwa Shelisheli mwezi Machi mwaka 2012 ikiwa na mateka hao.

    Mateka hao ambao wote ni wanaume wanatoka China, Philippines, Indonesia na Vietnam.

    Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje wa China Bibi Hua Chunying amethibitisha habari hiyo, na kusema kati ya mateka hao 10 wanatoka China Bara na wengine wawili wanatoka mkoa wa Taiwan. Pia amesema mateka mmoja kutoka China bara na mmoja kutoka Taiwan walipoteza maisha yao. Kwa sasa mateka hao 26 wamewasili nchini Kenya.

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang amesema, serikali ya China siku zote inashikilia kanuni za "kuwapa kipaumbele watu na diplomasia iwafanyie kazi watu, na kufanya usalama wa maisha ya mabaharia waliotekwa nyara kuwa kipaumbele cha kwanza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako